Sambaza

Maua Sama – Sijausikia Wimbo Wa Alicia Keys, Diamond

MSANII wa Bongo Fleva, Maua Sama , amefunguka #BONGO255 @255globalradio “Ninaandaa vitu vyangu by next month tutaanza kuachia, hapo nyuma kulikuwa na corona na sasa ni uchaguzi, kwa hiyo vimekwamisha mambo mengi, kulikuwa na albums, EPs ambazo zinahitaji international collaborations, lakini lockdown imeharibu, kwa sasa tunasubiri muda tu.
_

“Kufanya shows kwenye majukwaa ya siasa imenisaidia ku-gain vitu vipya, kuwa karibu na mashabiki na kuonyesha mazuri ambayo Rais wetu, Dkt. Magufuli ameyafanya kwa Taifa letu. Najua kuna wasanii wengi Afrika Mashariki lakini nashukuru kuchaguliwa kuwania Tuzo za AFRIMA, hili ni jambo kubwa sana kwangu.

“Nimeimba sana nyimbo za Jide Jaydee kabla sijatoka kimziki, ni msanii mzuri na kila msanii mwanamke anatamani kuwa kama yeye, nitafurahi siku moja nikitimiza ndoto yangu ya kupata Tuzo ya Grammy, itanisaidia kunipaisha kimataifa,” amesema Maua Sama.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey