Sambaza

Kanye West: Nitainunua Universal Music Group

MSANII Kanye West ameendelea kutoa kauli tata ambazo zimeendelea kugusa hisia za wengi. Baada ya kutupa tuzo za Grammy chooni sasa amesema kuwa atanunua kampuni ya kuuza na kusambaza muziki ya Universal Music Group.

Kampuni hiyo kongwe imefanya kazi na mamia ya mastaa tangu kuanzishwa kwake wakiwepo kina Bob Marley, Travis Scott, Lady Gaga, Jay Z, Tory Lanez, Rihanna, Lil Wayne, Diamond Platnumz, Adele, Tiwa Savage na hata Kanye West mwenyewe.

Lakini mbali na ukubwa wa kampuni hii bado Kanye West anaamini kuwa atanunua kaampuni hiyo ambayo inathamani ya Dola za Marekani Bilioni 33.

“Nitainunua Universal, ni kampuni yenye thamani ya Dola Bilioni 33 tu na mimi ni prodyuza bora aliyewahi kutokea duniani na bado ni mdogo nina miaka 43 tu, nitainunua,” Alisema Kanye West kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari.

Mbali na hayo pia Kanye West ameelezea suala la yeye kuonekana kama mgonjwa wa akili na amejibu na kusema, “Inafunga uwezo wa mimi kufanya kile anachotaka Mungu nifanye, ilifanya nisijiamini, nakumbuka niliwahi kusema ‘Utumwa ni Kuchagua’ na wakanitibu akili kisa nimesema hivyo.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey