Sambaza

Harmonize: ‘Halina Meno Hilo Simba Zee”

USIKU wa kuamkia leo Novemba 2, Harmonize, amefanya ‘party’ maalumu ya kutambulisha wimbo wake mpya unaoitwa Ushamba.

Katika seherehe hiyo, Konde Boy, alitupia baadhi ya mistari ambayo inaaminika kuwa ipo kwenye wimbo wake mpya ambapo moja ya mstari aliouimba Harmonize ni pamoja na huu unaosema “Limechoka acha tuligaragaze, halina meno hilo samba zee…”

Mashabiki mbalimbali wameamua kujiongeza wenyewe na kuhusisha mstari huo na aliyekuwa bosi wa Harmonize, Diamond Platnumz, ambaye inafahamika kuwa pia hujiita SIMBA.

Wimbo huo wa Ushamba ulitarajiwa kutoka jana lakini kwa mujibu wa Harmonize, amesitisha kuutoa mpaka leo kutokana na matatizo ya kimtandao yanayoendelea nchini.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey