Sambaza

Trump Amwagia Sifa Lil Wayne

 

Baada ya Lil Wayne kuweka wazi upande anaouunga mkono kwenye uchaguzi mkuu wa Marekani ambapo amesema atampigia kura Rais Donald Trump, Trump naye ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii huyo na kumuita mwanaharakati.

Rais Trump ameyasema hayo alipofanya mahojiano na kituo kimoja cha habari ambapo amesema “Ni mtu mzuri sana, mwanaharakati mwenye mawazo chanya na aliomba tuonane na nikakubali na kama mlivyoona kikaao kilienda vizuri sana.”

Lil Wayne aliwashtua watu wengi baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na Rais Trump na kuandika “amesikiliza tulichotaka kumuambia na amesema anaweza na atakamilisha jambo hilo.”

Hata hivyo wasanii mbalimbali walioneshaa wazi kutofurahishwa na kitendo hiko akiwemo 50 Cent ambaye alisema “Hapana Wayne, ingekuwa mimi nisingepiga picha na huyu bwana.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey