Alicia Keys Amwagia Sifa Diamond Platnumz
Mshindi wa tuzo za Grammy mara kadhaa, Alicia Keys, amemsifu msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, kwa aina yake ya uimbaji ambayo ameiita ya kipekee.
Alicia ameyasema hayo alipokuwa akifanya tathmini ya album yake aliyoitoa siku za karibuni ambapo Diamond ameshiriki kwenye wimbo uitwao ‘Wasted Energy.’
“Nimependa Diamond kuwa sehemu yaa album yangu, msanii wa Tanzania mkali ambaye ameibariki album yangu kwa aina yake ya uimbaji ya kipekee,” alisema Alicia Keys.
Diamond Platnumz ameweka historia ya kuwa Muafrika wa kwanza kushiriki kwenye album ya msanii wa Marekani.
Toa Maoni Yako Hapa