Sambaza

The Game – “Drake Ni Micheal Jackson Wa Hip Hop”

Nguli wa Muziki wa Hip Hop, The Game amempa heshima kubwa Rapa Drake kwa kumfananisha na mfalme wa Pop, Micheal Jackson.

The Game amesema hayo alipokuwa akijadili uwezekano wa kushindana na 50 Cent ambapo alisema kuwa kuna msanii mmoja tu ambaye album zake zimeshika namba moja mara nyingi kwenye chati za muziki kuliko yeye na sio mwingine bali Drake.

“Drake ndio msanii pekee aliyenizidi kwa kuwa na album namba moja , nadhani Drake ana album kumi zilizoshika namba moja” alisema The Game na kuongeza kuwa “Drake yupo vizuri ni kama Micheal Jackson wa Hip Hop.”

Hii sio mara ya Kwanza kwa Drake kufananishwa na mfalme wa Pop Micheal Jackson ambapo Fat Joe pia amewahi kufanya hivyo  pia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey