Sambaza

Meneja Akanusha Davido, Burna Boy Kupigana

MENEJA wa Twist Club iliyopo Ghana ambapo inasemekana hapo ndipo Davido na Burna Boy walipooonekana wakizozana amezungumzia tukio hilo.

Kwa mujibu wa meneja huyo ambaye hakukataa wala kukubali kama ni kweli Davido na Burna Boy walipigana amepinga vikali kuwa wasanii hao walikuwepo ndani ya klabu yake na badala yake amesema walikuwa kwenye klabu iliyopo jirani nao iitwayo ‘Level Up Rooftop Lounge.’

Kupitia mitandao ya kijamii uongozi wa Twist Club uliandika tamko la kukanusha kuwepo kwa wasanii hao kwenye klabu yao.

“Sisi kama kampuni tunabaki na msimaamo wa kutoa burudani kwa yeyote anayetaka kufurahia utajiri wa burudani ya Ghana katika mazingira salama na yenye ulinzi,” walimalizia uongozi wa Twist Club.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey