Young Thug – ‘Jay Z Hanifikii’
Rapa Young Thug amewaudhi baadhi ya mashabiki baada ya kusema kuwa ana nyimbo nyingi maarufu kuliko Jay Z.
Akifanya Mahojiano na mtangazaji Gillie Da Kids, Thug amesema kuwa anapofanaya shoo huwa ukumbi mzima unaaimba nyimbo zake na hata akipafomu nyimbo 30 basi ukumbi mzima utaimba nyimbo hizo.
“Ninapopafamu, ninakuwa na nyimbo 30 ambazo uwanja mzima utaziimba nyimbo zote,” alisema Thug na kuendelea “Hata Jay Z hana nyimbo hizo.”
Hata hivyo Thug alijitetea baada ya mtangazaji kusema kuwa hata Jay Z ana nyimbo nyingi kali. “Najua ata Jay Z ana nyimbo kali hata 50 lakini najaribu kusema wapo wengi ambao hawana nyimbo hizo,” alisema Young Thug.
Mashabiki hawajapenda kauli ya msanii huyo na kumuvaa kwenye mitandaao ya kijamii na kusema anatakiwa siku moja aingie kwenye shoo ya Jay Z aone watu wanavyoimba kila mstari.