Manchester United yatoa taarifa ya kuumia kwa Paul Pogba
Baada ya kuwa na mchango mkubwa kwa United kuongezeka kwa msimamo katika kipindi cha sikukuu na wakati wa mwezi wa ufunguzi wa 2021, Pogba alipata jeraha la paja katika sare ya 3-3 na Everton na alitolewa katika kipindi cha kwanza.
Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa supastaa huyo wa Ufaransa atakosekana kwa muda.
“Ni jeraha ambalo litachukua wiki chache kupona,” Solskjaer alisema. “Ameanza matibabu, akifanya kazi na wafanyakazi wa tiba na tutamrudisha haraka na salama iwezekanavyo. Kwa kweli, Paulo amekuwa muhimu sana kwetu na hatutakua na uzembe wowote. [Kwa hivyo ni] Wiki chache hakika. ”