Chris Brown Aburuzwa MAHAKAMANI, Kisa Mbwa
Msanii Chris Brown ameshtakiwa na mfanyakazi wake, Patricia Avila kwa madai kwamba mbwa wa msanii huyo alimshambulia na kumjeruhi dada wa msanii huyo aitwaye Maria, tukio lililotokea Desemba 12, 2020.
Inaelezwa kwamba mbwa wa Chris Brown, walikuwa wakifugwa katika eneo tofauti ndani ya makazi ya Chris, mahali ambapo hawakuwa wakionwa na wafanyakazi hao.
Inaelezwa kwamba siku ya tukio, mmoja kati ya mbwa hao, aliachiwa na kuelekea upande mwingine wa jengo hilo, ndipo alipokutana na Maria ambaye alikuwa akiendelea na shughuli za usafi ndani ya mjengo wa msanii huyo na kusababisha tukio hilo.
Mfanyakazi huyo anaeleza kwamba baada ya kusikia kelele za dada yake kuomba msaada, alikimbilia eneo la tukio ambapo alimkuta dada yake huyo akiwa amelowa kwa damu kutokana na shambulio hilo huku akiwa na majeraha usoni na kwenye mguu wake mmoja, harakaharaka akapiga simu kwa namba ya dharura ya 911.
Patricia anazidi kueleza kwamba dada yake huyo alilazimika kulazwa kwa siku kadhaa hospitali ambapo alifanyiwa upasuaji mara mbili hivyo anataka Chris Brown awalipe kiwango cha fedha ambacho hakijaelezwa wazi, kama fidia kutokana na madhara aliyoyapata dada yake huyo.