Sambaza

SNOOP DOGG; MUNGU Amemchukua MALAIKA Wake DMX

Msanii maarufu wa Hip Hop duniani, Snoop Dogg amesema kifo cha swahiba wake wa siku nyingi katika game la Hip Hop, Earl Simmons ‘DMX’ ni kama Mungu ameamua kumchukua malaika wake ili wakakae pamoja mbinguni.

Katika mahojiano yake na kipindi cha runinga cha Today, Snoop ambaye alichuana vikali na DMX katika shindano la kurap la Verzuz miezi kadhaa iliyopita, amesema licha ya mapungufu ya kibinadamu aliyokuwa nayo DMX, aliishi maisha ya kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kama alivyoagizwa na Mungu wake.

“Siku zote alikuwa anafanya kitu sahihi kwa wakati sahihi, alikuwa anawasaidia sana watu na hiyo inanifanya niamini kwamba Mungu ameamua kumchukua malaika wake na kumrudisha nyumbani.

Tangu kifo cha DMX kilichotokea April 9, 2021 Snoop amekuwa akituma meseji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, kuonesha namna alivyoguswa na kifo cha staa huyo wa Hip Hop.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey