Sambaza

Hatimaye PRINCE PHILIP Azikwa na Watu 30 Jijini London

 

Hatimaye Prince Philip, Mtawala wa Edinburg na mume wa Malkia Elizabeth, amezikwa katika mazishi ya kifamilia yaliyofanyika katika Kanisa la St George jijini London.

Katika mazishi hayo, kiongozi wa kidini wa Windsor alitoa risala ya kuuenzi ukaribu, ucheshi na utu huku waombolezaji wachache wapatao 30 wakiwa wamevalia barakoa na kukaa mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona wakihudhuria mazishi hayo.

Jeneza lake lilibebwa kwa mwendo mfupi hadi kanisa la St George kwa kutumia gari aina ya Land Rover, ambalo mtaalamu huyo alichangia katika kulifanyia marekebisho ya muundo wake.

Zaidi ya wanajeshi 730 walishiriki katika tukio hilo la kumuaga kisha kumzika kiongozi huyo aliyefariki April 9, 2021 katika Kasri la Windsor akiwa na umri wa miaka 99.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey