Sambaza

Shigongo Amzungumzia Hayati Magufuli na Rais Samia

Mbunge wa Buchosa na Mkurugenzi wa Global Group Ltd, Eric Shigongo amesema japokuwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli amefariki, bado ataendelea kuishi kwenye mioyo ya Watanzania kutokana na mambo mazuri aliyowafanyia!

Shigongo ameyasema hayo katika mahojiano maalum yaliyofanywa na Kituo cha Global TV Online na 255 Global Radio na kuongeza kwamba anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi alivyoyapokea majukumu ya kuiongoza Tanzania baada ya kifo cha Hayati Magufuli.

“Nimpongeze mama yetu Samia Suluhu Hassan, mwanamke wa shoka, ambaye kwa kuanza kwake kuingoza nchi yetu amefufua matumaini ya Watanzania baada ya kumpoteza aliyekuwa Rais wetu, Dkt. John Magufuli,” amesema na kuongeza:

“Mambo yote aliyoyaanzisha Hayati Magufuli yatatekelezwa na Mama Samia, sababu Ilani ya CCM ipo na kinachotekelezwa ni Ilani ya CCM. Hawa wote walikuwa timu moja na lengo lao lilikuwa moja, hakuna kilichobadilika. Mama yupo.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey