Sambaza

RAIS WA CHAD AUAWA NA WAASI MUDA MFUPI BAADA YA KUSHINDA UCHAGUZI

 

Rais wa Chad, Idriss Deby amefariki dunia saa chache baada ya kutangazwa kushinda uchaguzi wa Urais kwa muhula wa sita.

Taarifa zilizotolewa na Jeshi la Chad na kutangazwa na redio ya taifa, Deby amefariki baada ya kupata majeraha kwenye mapambano dhidi ya waasi wanaoshambuliana na majeshi ya serikali, wakijaribu kuuteka mji mkuu, N’Djamena.

Taarifa zinaeleza kwamba baada ya matokeo kutangazwa na kuonesha kwamba Rais Deby ameshinda kwa asilimia 79.3 katika uchaguzi mkuu uliofanyika April 11, mwaka huu, aliamua kwenda kuungana na jeshi la nchi hiyo kupambana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo ambako kwa bahati mbaya, alijeruhiwa na baadaye kupoteza maisha.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey