Sambaza

PROFESA JAY: NINA NDOTO ZA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo na aliyekuwa Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay, amesema anazo ndoto za kuja kugombea urais wa Tanzania na kwamba kutokuwepo kwake bungeni katika awamu hii, hakujazikatisha ndoto zake hizo.

Akizungumza katika kipindi cha 255 Bongo kinachorushwa na Kituo cha Redio cha +255 Global Radio, Profesa Jay amesema anachoamini ni kwamba katika uchaguzi mkuu wa 2020, alishinda ubunge wa Mikumi lakini hakutangazwa na kuongeza kwamba bado anazo ajenda zake katika jimbo hilo ambazo bado hazijakamilika.

“Nitagombea tena mwaka 2025 na pengine inaweza isiwe ubunge tu bali urais kwa sababu nina ndoto kubwa katika siasa,” alisema Profesa Jay.

Kuhusu masuala yanayoikabili gemu ya Bongo Fleva, Profesa Jay amesema umefika wakati wasanii wa muziki wanapaswa kuachana na mwenendo mbovu wa kutunga mashairi yenye lugha zisizofaa kwa jamii kwa sababu wanaurudisha nyuma muziki wa Bongo Fleva ambao yeye na wenzake waliupambania miaka mingi nyuma kuhakikisha unapanda chati.

Akizungumzia sakata la msanii Harmonize na Rayvanny kuchafuana mitandaoni, Profesa Jay amewaasa kuachana na kiki zisizo na maadili na badala yake waelekeze nguvu zao katika kufanya muziki mzuri ambao utawafurahisha mashabiki na kuielimisha jamii.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey