Sambaza

RAIS SAMIA ATEMA CHECHE BUNGENI

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaonya watu wote ambao wanaodhani kwamba Hayati Dk. John Pombe Magufuli ameondoka na mipango yake ya usimamizi wa mali za umma, kupambana na ukwepaji kodi, kuziba mianya ya kupoteza mapato, kukemea uzembe na wizi na kusisitiza kwamba serikali yake itaendelea na mipango hiyo kama alivyoianzisha Hayati Magufuli.

Rais Samia ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma, wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza dira ya serikali yake, katika kuwaletea wananchi maendeleo ambapo amesisitiza kwamba serikali yake haitarudishwa nyuma katika mapambazo dhidi ya watu wanaochezea rasilimali za nchi.

Pia Rais Samia amekemea vikali watu wanaotumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa za uchonganishi kuhusu kifo cha Hayati Magufuli wakidai alipewa sumu au kuwekewa vitu vilivyosababisha kifo chake na kuwataka waache mara moja vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Rais Samia amesisitiza kwamba taarifa ya madaktari inaeleza kwamba kifo cha Magufuli kilisababishwa na tatizo la udhaifu wa moyo aliloishi nalo kwa takribani miaka kumi na kuwataka watu wanaoeneza taarifa za uchonganishi mitandaoni, kama waoa ushahidi, waupeleke kwa vyombo vya uchunguzi badala ya kuzisambaza mitandaoni.

Mambo mengine yaliyozungumwa na Rais Samia katika hotuba yake hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wastaafu, ni pamoja na serikali kurudisha imani kwa wawekezaji na kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje, ikiwa ni pamoja na kuunda sera nzuri, kusimamia ulipaji rafiki wa na kupunguza urasimu serikalini.

Pia ameeleza kwamba serikali itaanzisha mchakato wa kuyapitia mashirika ya umma ili yaweze kujiendesha kwa faida, serikali itakutana na wadau wa sekta binafsi na kuangalia namna ya kufanya nao kazi kwa tija ikiwa ni pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji nchini.

Pia amesema serikali ipo kwenye mpango wa kuhakikisha inalilea shirika la ndege ATCL kimkakati kwa kufanya uchambuzi wa kina kuhakikisha shirika hilo linajiendesha kwa faida.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey