Sambaza

SHEREHE YA NDOA YA MAJIZZO NA LULU YANUKIA

BAADA ya msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mmiliki wa kituo cha EFM na TVE, Francis Ciza ‘Majizzo’ kufunga ndoa ya kimyakimya, inadaiwa kuwa wawili hao wapo kwenye mipango ya  kuangusha bonge la sherehe.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu na wanandoa hao, wawili hao wapo kwenye mipango ya  kufanya sherehe kubwa itakayoacha watu midomo wazi.

Hata hivyo, bado haijafahamika sherehe hiyo itafanyika wapi na lini lakini ni baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Akizungumza kupitia TVE hivi karibuni, Majizzo alisema waliamua kufunga ndoa hiyo bila kufanya sherehe kubwa kwa ajili ya kuwatia moyo vijana kwamba kuoa si lazima uwe na uwezo mkubwa wa kifedha.Alisema mara baada ya kufunga ndoa kanisani, kila mmoja alishika njia yake na kwenda kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Februari 16, mwaka huu Lulu na Majizzo walifunga ndoa ya siri katika Kanisa la Katoliki la Mt. Gasper lililopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Ndoa yao ilikuwa gumzo sana kutokana na usiri walioamua kuufanya ambapo siku hiyo, waandishi mbali na vyombo vya Majizzo vya habari, walizuiwa kuchukua matukio kanisani hapo huku ulinzi ukiwa mkali.

STORI: MEMORISE RICHARD

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey