Sambaza

Mchekeshaji Kansiime Ajifungua Mtoto wa Kiume

Mchekeshaji maarufu toka nchini Uganda, Anne Kansiime amejifungua mtoto wa kiume jana Jumamosi Aprili 24, 2021 na kumpa jina la Selassie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anne (34) alithibitisha kujifungua kwa ku-share picha inayomuonyesha akiwa kitandani ndani ya hospitali aliyojifungulia mwanae huyo, akionekana kumbembeleza na kusema kuwa anaitwa “Selassie Ataho”.

Pia aliongeza maneno yanayosomeka, “dhambi zake zimesamehewa” Hii ni kama amewakata ngebe mahasimu wake, baada ya kuandamwa kwa muda mrefu na maneno ya kuwa hawezi kushika ujauzito.

Selassie anakuwa mtoto wa kwanza kwa Kansiime na mpenzi wake Abraham Tukahiirwa ‘Skylanter’.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey