Sambaza

SHIGONGO AWASILISHA RIPOTI YA KAMATI YA MAZINGIRA BUNGENI

Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia Mazingira kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimetakiwa kushirikiana kudhibiti uingizwaji holela na matumizi ya kemikali hatarishi ya zebaki nchini, kwani kemikali hiyo imekuwa na madhara makubwa kwa afya za wananchi hususan wachimbaji wadogo wa dhahabu pamoja na mazingira.

Ushauri huo umetolewa leo bungeni na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Eric Shigongo wakati akiwasilisha mapendekezo ya kamati hiyo ya bunge kwa serikali.

Shigongo amesema wachimbaji wadogo wa madini huitumia kemikali hiyo kusafishia madini bila kuwa na vifaa maalum vya kujikinga hivyo kuhatarisha afya zao, huku maji yake yakitiririka kwenye vyanzo vya maji na kuingia kwenye mito na maziwa, hivyo kuathiri mazingira sambamba na afya za wananchi wanaotumia maji hayo.

Mapendekezo mengine yaliyotolewa na kamati hiyo, ni pamoja na kuwepo kwa mfumo wa kitaasisi wa usimamizi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuanzisha vitengo vya usimamizi wa mazingira kwenye kila taasisi na sekta kuanzia ofisi ya rais mpaka serikali za mitaa sambamba na serikali kuuwezesha mfuko wa taifa wa dhamana ya hifadhi ya mazingira ili uanze kufanya kazi.

Pia kamati hiyo imeshauri serikali kuongeza utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi, kufanya mapitio na maboresho ya sera ya taifa ya mazingira ya mwaka 1997 ambayo inaonesha kupitwa na wakati pamoja na upatikanaji na utumiaji wa nishati mbadala, ikiwemo mkaa unaotengenezwa kutokana na takataka pamoja na kuongeza upandaji wa miti nchi nzima.

Kamati hiyo pia imependekeza kufanyika kwa tathmini ya athari za mazingira kabla ya mradi wowote kufanyika na kulitaka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC kusimamia kwa karibu tathimini hiyo ili kupunguza urasimu wakati wa uanzishaji wa miradi mipya ya maendeleo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey