Sambaza

URAIA WA MKENYA ALIYESHINDA TUZO ZA OSCAR GUMZO

Usiku wa Jumapili, April 25, 2021, zilifanyika sherehe za utoaji tuzo za Oscar nchini Marekani ambapo msanii kutoka Kenya, Daniel Kaluuya alishinda tuzo ya ‘Best Supporting Actor’, ikiwa ni mara yake ya kwanza kushinda tuzo hiyo kupitia Filamu ya Judas and The Black Mesiah.

Ushindi huo umewafanya wengi kuanza kumfuatilia kwa karibu, wakitaka kujua historia yake. Licha ya kwamba ana uraia wa Kenya na Marekani, Kaluuya mwenye umri wa miaka 32, alizaliwa jijini London na inaelezwa kwamba wazazi wake, akiwemo baba yake na mama yake, Damalie ni raia wa Uganda.

Kitendawili ambacho bado hakijapatiwa majibu mitandaoni, ni vipi mwigizaji huyo anatajwa kuwa raia wa Kenya wakati hakuzaliwa Kenya wala wazazi wake hawana asili ya nchi hiyo? Ni muda ndiyo utakaotoa majibu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey