Sambaza

LICHA YA TREY SONGZ KUZICHAPA NA POLISI, HATAFIKISHWA MAHAKAMANI

Msanii mkubwa wa RnB kutoka nchini Marekani, Tremaine Aldon Neverson almaarufu Trey Songz hatafikishwa mahakamani kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha, baada ya Jumapili iliyopita kuzichapa na afisa wa polisi aliyekuwa akitaka kumkamata.

Mike Mansur ambaye ni msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Jackson County, amesema licha ya kuwepo kwa ushahidi wa video unaomuonesha msanii huyo akirushiana ngumu na polisi katika mechi kati ya Timu za Kansas City Chiefs dhidi ya Buffalo Bills Jumapili iliyopita, hakuna ushahidi mwingine wa kutosha unaoweza kuwafanya polisi wamfikishe mahakamani.

Kipande cha video kilichosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, kinamuonesha Trey Songz akivutaka kasha kurushiana ngumi na askari aliyekuwa akitaka kumkamata, kwa sababu ambazo bado hazijafahamika, tukio lililotokea kwenye Uwanja wa Arrowhead.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey