Sambaza

SAMIA: SERIKALI HAINA UWEZO WA KUONGEZA MISHAHARA KWA SASA

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema licha ya serikali kutoongeza mishahara kwa muda wa miaka sita kwa wafanyakazi wa umma, kwa sasa serikali haina uwezo wa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma kwa sababu mbalimbali, ikiwemo janga la Corona lililosababisha uchumi wa nchi ushuke kutoka asilimia 6.9 hadi asilimia 4.7 na kuahidi kwamba atafanya hivyo katika mwaka ujao wa fedha.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Pia Rais Samia ametangaza kushusha kiwango cha kodi kinachokatwa kwenye mishahara ya watumishi wa umma (PAYE), kutoka asilimia tisa ya sasa hadi asilimia 8 na kuahidi kwamba serikali itawapandisha madaraja wafanyakazi kati ya 85,000 hadi 91,000, italipa malimbikizo ya zaidi ya shilingi bilioni 60 wanayodai wafanyakazi na kuajiri watumishi wapya wapatao 40,000.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey