Sambaza

H-BABA; DIAMOND AACHE KUDANGANYA, HANA UWEZO WA KUNUNUA NDEGE

Msanii wa kitambo wa Bongo Fleva, H-Baba amemshukia Diamond Platnumz kwa kumtaka aache kuwadanganya mashabiki wake kwamba amenunua ndege binafsi (private jet) kwani si kweli na hana uwezo huo.

Akipiga stori katika Kipindi cha Katambuga kinachorushwa na kituo cha redio cha +255 Global Radio, H-Baba amesema Diamond na ‘menejimenti’ yake waache kuzungumza uongo kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kwani kwa kufanya hivyo, wanawaharibia maisha vijana wengi.

Amesema wapo vijana wengi ambao wameamua kuachana na masomo yao wakiamini kwamba wanaweza kufanikiwa kwa urahisi kupitia muziki kama Diamond, jambo ambalo siyo kweli na kulitaka Baraza la Sanaa (Basata) kukemea vitendo hivyo.

Amesisitiza kwamba endapo ni kweli Diamond amenunua ndege hiyo na endapo ikitua nchini, yupo tayari kutembea kwa miguu akiwa mtupu kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Kauli hiyo ya H-Baba, imekuja siku chache baada ya picha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikimuonesha Diamond na mameneja wake wakiwa ndani ya ndege ambayo ilidaiwa kwamba imenunuliwa na Diamond.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey