Sambaza

BRITNEY SPEARS AMKATAA BABA YAKE, KUMBURUZA MAHAKAMANI

Bifu kati ya mkali wa RnB wa kitambo nchini Marakeni, Britney Spears na baba yake mzazi, Jamie umechukua sura mpya baada ya msanii huyo kukataa kuendelea kusimamiwa na baba yake na kuanza mipango ya kumfikisha mahakamani, akitaka atolewe katika nafasi ya uangalizi wa mali zake.

Kwa zaidi ya miaka 13 sasa, Jamie amekuwa ndiye msimamizi wa mali na matumizi yote ya Britney, kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuzuia mwanaye huyo asifilisike kutokana na matumizi mabaya ya fedha ambayo amekuwa nayo kwa kipindi kirefu.

Kwa mujibu wa Mtandano wa TMZ, Britney amesema amechoshwa kuchungwa na baba yake huyo kwani amekuwa akimnyima uhuru wa kutumia fedha zake kama mwenyewe anavyotaka na ametishia kwamba hatajihusisha na masuala yoyote ya muziki mpaka baba yake huyo atakapoondolewa na mahakama kwenye nafasi hiyo.

Jamie aliamua kuwa msimamizi wa mali za mwanaye, kutokana na tabia ya Britney kutumia fedha hovyo, wakati mwingine akinunua magari ya kifahari mpaka matatu kwa mpigo, jambo ambalo alisema lingesababisha mwanaye huyo kufilisika, suala likapelekwa mahakamani na hatimaye akashinda na kuwa msimamizi rasmi wa mali zote za mwanaye pamoja na matumizi yake.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey