Sambaza

PICHA ZA AKA AKIMSHAMBULIA MPENZI WAKE HOTELINI ZAVUJA

Picha za msanii maarufu nchini Afrika Kusini, Kiernan Forbes ‘AKA’ zimevuja zikimuonesha akiwa anamshambulia mpenzi wake, Anele Tembe takribani mwezi mmoja kabla mrembo huyo hajachukua uamuzi wa kuyakatisha maisha yake kwa kujirusha kwenye jengo la ghorofa 15 mpaka chini.

Katika picha hizo zinazotajwa kuvujishwa na mmoja kati ya marafiki wa karibu wa Anele, zinamuonesha AKA akivunja mlango wa chumba cha mwanadada huyo, ambaye inaelezwa aliamua kujifungia ndani baada ya mpenzi wake huyo kumshushia kichapo.

Inaelezwa kwamba uhusiano wa kimapenzi wa wawili hao, ulijawa na vurugu kubwa, AKA akidai kwamba ni kwa sababu mpenzi wake huyo alikuwa akitumia madawa ya kulevya, huku marafiki na familia yake wakikanusha madai hayo.

Inazidi kuelezwa kwamba AKA ndiye aliyekuwa akitumia madawa ya kulevya ambayo yalikuwa yakimchanganya kichwa nakumfanya amfanyie matukio ya ukatili mpenzi wake huyo.

Polisi wa Afrika Kusini, wanaendelea na uchunguzi wa video hizo, ili kubaini kama AKA alikuwa chanzo cha kifo cha mrembo huyo aliyefariki April 11, mwaka huu kwa kujirusha kutoka ghorofa ya 15 katika hoteli moja jijini Cape Town.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey