Sambaza

Fainali ya Uefa Champions League Kupigwa Ureno

SHIRIKISHO la soka barani Ulaya , UEFA limethibitisha kwamba mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Chelsea dhidi ya Manchester City itapigwa nchini Ureno na sio tena Uturuki kama ilivyokuwa imepangwa.

Awali mechi hiyo ilipangwa kupigwa katika jiji la Istanbul na sasa itapigwa uwanja wa nyumbani wa  klabu ya FC Porto , Estadio do Dragao, tarehe ikiwa ile ile ya Mei 29, 2021.

Serikali ya Uingereza imeiweka Uturuki kwenye orodha ya nchi ambazo zina maambukizi makubwa ya virusi vya corona hali iliyopeleke fainali huiyo kuhamishiwa Ureno.

Estadio do Dragao una uwezo kuchukua mashabiki 50,000 na UEFA wapo kwenye mazungumzo na Serikali ya Ureno kuruhusu mashabiki 20,000 kuhudhuria fainali, huku kila klabu itaruhusiwa mashabiki 6,000

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey