Sambaza

Kisa Simba, Mo Dewj Aahirisha Kununua Royce Rolls, Ferrari

Mo, Simba, Kaizer ChiefsKufuatia kipigo cha mabao 4-0 walichokipata mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba Sport Club katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa dhidi ya Timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameahirisha mpango wake wa kujizawadia magari aina ya Ferarri na Rolls Royce.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo amesema ameamua kuachana na mpango wake huo ambapo fedha hizo atazielekeza katika Klabu ya Simba.

“Nilipanga kujizawadia Ferrari na Rolls-Royce, sina budi kuweka mpango huu kapuni kwa sasa na kuelekeza fedha zaidi katika klabu yetu ya SimbaSC. Furaha ya Simba SC Tanzania ni muhimu kuliko starehe yangu. Simba kwanza!”

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey