Sambaza

MZEE YUSUF AELEZA ALIVYOTAITIWA NA POLISI

Kufuatia kusambaa kwa picha inayomuonesha msanii mahiri wa Taarab, Mzee Yusuf akiwa amekamatwa na polisi na kufungwa pingu, msanii huyo ametoa ufafanuzi na kueleza kuwa ni kweli alikamatwa na polisi kwa kesi ambayo mtuhumiwa hakuwa yeye.

Ameeleza kwamba kilichosababisha akakamatwa na polisi, ilikuwa ni kushindwa kufika kituo cha polisi alikoitwa kwa zaidi ya mara tano, jambo lililowalazimu askari kutumia nguvu kwenda kumkamata.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio, Mzee Yusuf ameeleza kwamba katika kesi ya msingi, wafanyakazi wake walimshambulia mtu mmoja mbele ya ofisi ya Mzee Yusuf, hivyo akawa anatakiwa kwenda kutoa maelezo kuhusu tukio hilo.

“Kuna jamaa alinishtaki kwa sababu amepigwa na wafanyakazi wangu mbele ya ofisi yangu, polisi wakanitumia wito lakini kwa sababu ya ubize nilishindwa kwenda, jambo lililosababisha wanifuate na kunikamata,” amesema Mzee Yusuf na kuongeza kuwa kwa sasa, anaendelea kuripoti polisi kama alivyoelekezwa ili kuweka mambo sawa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey