Sambaza

MAHAKAMA Yaukataa Wosia wa Mengi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeukataa wosia uliokuwa ukidaiwa kuandikwa na aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, marehemu Reginald Mengi pamoja na mambo mengine ikieleza kuwa haukidhi matakwa ya kisheria ili kuwa wosia halali.

Mahakama hiyo imeeleza kwamba wosia uliandikwa na Mengi akiwa tayari mgonjwa na hayuko sawa kiakili ambapo mahakama imeamua kuwa Mengi hakuwa sawa kiakili tangu mwaka 2016, wosia umewanyima urithi watoto halali bila sababu za msingi na marehemu amegawa mali nyingine ambazo siyo zake peke yake hivyo imeamriwa mahakamani hapo kuwa wasimamizi wa mirathi wawe ni mtoto wa marehemu, Abdiel Mengi na kaka wa marehemu, Benjamin Mengi.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Yose Mlyambina kufuatia shauri la mirathi lililokuwa limefunguliwa na watu wanne wakiwemo ndugu wa marehemu, wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey