MBUNGE WA KONDE, ZANZIBAR AFARIKI DUNIA
Mbunge wa Jimbo la Konde, Pemba visiwani Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Khatib Haji amefariki dunia alfajiri ya leo, Mei 20, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Kifo cha mbunge huyo kimethibitishwa na Katibu wa Idara ya Bunge, Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, Hamad Yussuf na kueleza kuwa mipango ya mazishi inaendelea na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF kuanzia 2010 hadi 2020 kabla ya kuhamia ACT Wazalendo na amewahi kuwa Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuanzia 1984 hadi 1987.
Toa Maoni Yako Hapa