Sambaza

BABA DIAMOND: Mwanangu Diamond Alinitumia Hela ya Eid

Mzee Abdul Jumaa maarufu kama Baba Diamond, amesema msanii mkubwa wa Bongofleva, Nasibu Abdul, alimtumia fedha za Sikukuu ya Eid el Fitr wiki chache zilizopita, jambo ambalo lilimfurahisha sana na kumfanya amsamehe kwa mambo yote yaliyotokea.

Mzee Abdul ambaye miezi michache iliyopita aliingia kwenye headline baada ya mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim almaarufu Sandra kutangaza hadharani kwamba yeye hakuwa baba mzazi wa msanii huyo, amesema ‘skendo’ hiyo ilimfanya akae ndani kwa zaidi ya miezi miwili.

“Nilikuwa nashindwa hata kutoka nje maana kila ninakopita nanyooshewa vidole… ila kwa sasa namshukuru Mungu mimi na Diamond mambo yanakwenda vizuri. Siku ya sikukuu, nikiwa sina hili wale lile, nilishangaa fedha zikiingia kwenye simu yangu, Diamond akanipigia simu, nikamuuliza wewe nani? Akajitambulisha, nikafurahi sana,” amesema Baba D wakati akifanyiwa mahojiano na Kipindi cha Hotpot kinachorushwa Global TV na +255 Global Radio.

Kupata mahojiano kamili, tembelea Global TV Online Youtube!

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey