Sambaza

Carlinhos Asitisha Mkataba na Yanga

Uongozi wa Klabu ya Yanga, umetangaza kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na mchezaji Carlos Stenio Fernandes do Carmo almaarufu kama Carlinhos kuanzia leo.

Katika taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mawasiliano ya Klabu ya Yanga, hatua hiyo imefuatia ombi la mchezaji huyo alilowasilisha kwa uongozi na baada ya majadiliano na kwa kuzingatia maslahi mapana ya pande zote mbili, wamefikia muafaka wa kusitisha mkataba.

Klabu hiyo imemshukuru Carlinhos kwa utumishi wake ndani ya klabu hiyo na kumtakia kila la heri katika maisha yake ya soka nje ya Klabu ya Yanga.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey