Sambaza

Dogo Janja Atamani Babaake Angekuwepo Ashuhudie Penzi Lake

STAA wa Hip Hop kutoka Arusha, Dogo Janja amesema anatamani marehemu baba yake mzazi angekuwepo hai na kushuhudia jinsi alivyobarikiwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja ametupia picha akiwa na mpenzi wake na kusindikiza na ujumbe huo akimaanisha endapo baba yake angekuwa hai, angempa furaha zaidi mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Quenlinna.

“Natamani marehemu baba yangu angekuepo aone how blessed he could be to have me! Ungeenjoy sana we binti,” aliandika Dogo Janja.
Mpenzi wake huyo naye akajibu hivi: “Usiseme hivyo hubby anatuona kila siku na nina imani tupo naye wakati wote na tushukuru Mungu tunaye mzee Jacob pia.”
Dogo Janja kabla ya kuwa na mahusiano hayo mapya na Quenlinna, aliwahi kudaiwa kufunga ndoa na muigizaji Irene Uwoya na kisha baadaye kuachana.

Credits:

@hotpot_tz

@erick.evarist

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey