Sambaza

NISHER: HANSCANA SIYO LEVEL ZANGU

Muongozaji video (dairekta) wa kitambo kwenye gemu la Bongo Fleva, Nisher amesema ni makosa kumlinganisha na dairekta mwingine, Hanscana kwa sababu siyo level zake.

Akipiga stori na kituo kimoja cha redio, Nisher amenukuliwa akisema yeye ndiye aliyemfundisha kazi dairekta mwingine, Khalfan Khalmandro ambaye ndiye mwalimu wa Hanscana na kueleza kuwa hatakiwi kuwa na ‘battle’ na Hanscana kwa sababu amefundishwa na mwanafunzi wake.

“Hanscana mimi hanihusu ila anayenihusu ni Khalfani ambaye ametoka kwenye mikono yangu kwa hiyo sitakiwi kuwa na battle na Hanscana ambaye ametoka kwenye mikono ya Khalfani Khalmandro, Hanscana sio level zangu,”  amesema Nisher.

Nisher na Hanscana wanatajwa kuwa kwenye bifu la chinichini, huku wadau wengi wa muziki, wakizishindanisha video zinazotengenezwa na madairekta hao wenye umaarufu mkubwa Bongo kutokana na kufanya video zenye ubora mkubwa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey