PRINCE HARRY NA MKEWE WAPATA MTOTO WA PILI
Mwanamfalme Harry na mkewe Mergan wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili, msichana. Lilibet “Lili” Diana Mountbatten-Windsor aliyezaliwa Ijumaa asubuhi katika Hospitali ya Santa Barbara, California.
Taarifa iliyotolewa na Kasri ya Buckingham inasema mama na mtoto wapo katika hali nzuri ya kiafya huku Harry na Meghan wakisema wamempatia mtoto wao wa pili jina la Lilibet ambalo ni jina la utani la Familia ya Kifalme kwa Malkia.
Jina lake la kati, Diana, limechaguliwa kumuenzi bibi yake, marehemu Princess Diana, Malkia wa Wales.
Toa Maoni Yako Hapa