Sambaza

Mr. P wa Kundi la P Square Ageukia Ufundi Makenika

Je, ameacha muziki? Hilo ndilo swali lililojitokeza miongoni mwa mashabiki Peter Okoye a.k.a Mr. P ambaye ni pacha wa Rude Boy au Paul Okoye ambao kwa pamoja walikuwa wakiunda kundi la P Square.

Swali hilo limetokana na picha alizozitupia katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram ambapo ameonekana akipambana kutengeneza injini ya gari katika gereji moja iliyopo nchini humo.

Mapacha hao ambao walitamba vilivyo miaka iliyopita na ngoma zao maarufu kama ‘Temptation’, walitengana kisha kila mmoja kuanza kuimba kivyake hali inayodaiwa kuchangia kudorora kwa muziki wao.

Hata hivyo, kuonekana kwa Mr. P katika shughuli hizo nzito za gereji mashabiki wamemtupia maswali na kumuuliza ameacha muziki na kuhamia kwenye ufundi wa magari lakini hadi sasa hajajibu kitu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey