Sambaza

ZUCHU Atwaa Tuzo YouTube

Mtandao wa YouTube umempa tuzo ya dhahabu (Gold Plaque) msanii wa Bongo Fleva, Zuhura Othman au Zuchu kwa kufikisha wafuatiliaji (subscribers) milioni moja (1,000,000) kwenye chaneli yake ya mtandao huo.

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye Mtandao wa YouTube ambao chaneli zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea.

Zuchu ambaye ana mwaka mmoja na miezi miwili tangu atambulishwe rasmi kujiunga na Lebo ya WCB Wasafi, Aprili 8, 2020, anakuwa msanii wa kwanza wa kike Bongo kufikisha Idadi hiyo kubwa ya wafuatiliaji.

Anayemfuata Zuchu YouTube kwa Bongo ni msanii mwenzake, Faustina Charles au Nandy ambaye anawafuatiliaji  781K. Wa tatu ni Christina Shusho mwenye 327K. wa nne ni Rose Muhando mwenye 300K na wa tano ni Vanessa Mdee mwenye 281K.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey