Sambaza

DIAMOND AWAJIBU WANAOTAKA ATOLEWE TUZO ZA BET

Staa wa Bongofleva na mmiliki wa Lebo ya Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amewajibu watu wanaotaka aondolewe kwenye tuzo za BET akisema ni mawazo yao na anayaheshimu.

Diamond ametoa kauli hiyo katika sherehe ya Krish, mtoto wa mwigizaji nyota wa filamu nchini, Irene Uwoya na kueleza kuwa anaheshimu mawazo ya kila mmoja.

“Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru,” amesema Diamond wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kwenye sherehe hiyo.

Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wakitaka atolewe kwenye tuzo hizo kwa kuwa hana vigezo, wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonesha hisia zao kutokana na msanii huyo kushiriki siasa na kutokemea matukio yanayowagusa moja kwa moja wananchi na kuwaathiri.

Diamond ameahidi kulizungumza suala la kupingwa kwake kwa kina zaidi siku chache zijazo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey