Sambaza

Wanandoa Wafariki Bafuni Afrika Kusini

Wanandoa hao wapya Zaheer Sarang na Nabeelah Khan (24) wamefariki dunia kwa shoti ya umeme huko Afrika kusini ikiwa ni siku moja tu tangu watoke kula fungate ‘honeymoon’

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa polisi wa jimbo la Guetang, Mavela Masondo alisema miili ya wanandoa hao iligunduliwa bafuni kwao Jumapili Juni 13, mwaka huu.

Ilisema wanandoa hao wakiwa bafuni mke huyo alishika tap/switch akapigwa na shoti ya umeme ambapo mume alipojitosa kumuokoa na yeye akaunganishwa katika shoti hiyo wakafariki wote.

Aidha, taarifa za awali zinaele kuwa maeneo hayo watu hupenda kujiunganishia umeme kiholela kinyume na sheria na hivyo kusababisha majanga kama hayo.

Hata hivyo, polisi wamesema bado wanaendelea kuchunguza zaidi tukio hilo kwa kushirikiana na mamlaka inayohusika kusambaza umeme katika jimbo la Guetang.

STORI NA MUSHI GABRIEL | GPL

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey