Sambaza

Ronaldo Kumfuata Messi Barcelona

Rais wa Barcelona, Joan Laporta amepanga kutimiza ndoto ya kuwakutanisha magwiji wa soka duniani Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika msimu ujao barani Ulaya.

Laporta ambaye alirejeshwa madarakani mapema mwaka huu amethibitisha kwamba yuko tayari kutoa ofa ya wachezaji watatu kwa klabu ya Juventus ambayo Ronaldo anachezea sasa ili kukamilisha dili hilo.

Wachezaji hao ni Antoine Griezmann, Philippe Coutinho na Sergi Roberto wanatarajiwa kutolewa kama chambo ili kuishawishi Juventus kumuachia Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno na mshindi mara tano wa Ballon d’Or.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey