King Kiba Afungukia Ishu ya Kununua Views Youtube
Mfalme wa Bongo Fleva, @officialalikiba anaendelea kukiwasha na ngoma zake kwenye platforms za muziki hasa Youtube ambako baadhi ya watu wametia maneno kwamba huwenda akawa ananunua watazamaji (viewers) kwenye mtandao huo.
Baada ya minong’ono hiyo mingi, mkali huyo anayekimbiza na Ngoma ya Saluti amefunguka kuhusu ishu hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, @officialalikiba amejibu moja ya ya ‘Tweet’ ya shabiki ambaye alimuandika; “Eti Alikiba ananunua views. Ila watu hampendi amani. Kisa amewapiga la mkono sio?”
Kwa upande wake @officialalikiba alimjibu kwa kusema; “Siwezi kujitekenya na kucheka mwenyewe.”
Toa Maoni Yako Hapa