TETESI: KLABU YA SIMBA YAIALIKA AL AHLY SIMBA DAY
Tetesi zinazosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ni kwamba kuelekea Tamasha la Simba Day linalotarajiwa kufanyika Jumapili ya Septemba 19, 2021 katika Uwanja wa Mpira wa Mkapa, Klabu ya Simba imeiandikia Klabu ya Al Ahly, kuja kucheza nayo mchezo wa kirafiki katika tamasha hilo.
Uongozi wa klabu ya Simba bado haujathibitisha taarifa hizo lakini gumzo limeendelea kuwa kubwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, huku taarifa nyingine zikieleza kwamba timu zilizopendekezwa na Al Ahly ya Misri au Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
Toa Maoni Yako Hapa