Vanessa na Rotimi watarajia kuwa wazazi kwa mara ya kwanza
Na Bakari Mahundu, Dar
Mwanamuziki na muigizaji wa filamu kama; The Power na Coming to America 2, Rotimi na mpenzi wake, Vanessa Mdee ambae ni muimbaji kutokea Tanzania, wanatarajia kuwa wazazi kwa kupata mtoto wao wa kwanza ambae wamethibitisha kuwa ni mtoto wa kiume!.
Wapenzi hao wawili, walivarishana pete ya uchumba mwishoni mwa Disemba, 2020 , wamefunguka jana , kupitia jarida la PEOPLE juu ya matarajio yao ya kupata mtoto wao wa kwanza!.
“Tunafurahi sana kumkaribisha mtoto wetu, Kama wazazi kwa mara ya kwanza, kila kitu juu ya uzoefu huu kimekuwa changamoto mpya kabisa“ Walisema kupitia mahojiano na jarida hilo.
Toa Maoni Yako Hapa