Sambaza

DONI ADAI KUMNUNULIA WEMA FERARI LA BILIONI MOJA

Na Bakari Mahundu, Dar

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii, hasa Instagram, basi utakuwa umekutana na stori zinazotrendi juu ya Doni anayedai kumpa Wema Sepetu gari aina ya Ferari  kama zawadi ya uchumba wao!.

Doni huyo anayefahamika kama Rashidi Mulumba maarufu kama PCK, katika mtandao wa Instagram, amezua gumzo baada ya kuonyesha aina ya gari ambalo amedai atamzawadia bidada Wema, ndani ya siku chache zijazo!

Global Redio na Global Publishers, ikamtafuta Mwamba huyo na kupiga nae stori mbili tatu juu ya ukweli wa suala analodai. Kupitia mahojiano na Global Publishers, Doni Mulumba, ama PCK alithibitisha kuwa amemnunulia Bidada wema gari hilo aina ya Ferari lenye thamani ya bilioni moja, ambalo litaingia nchini ndani ya siku chache zijazo, huku akiweka bayana kuwa ana miliki magari kama hayo ya kutosha tu!.

Full Interwiew itakujia kupitia gazeti la IJUMAA

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey