WATANZANIA KUPEPERUSHA BENDERA ,AFRIMA
Na Bakari Mahundu, Dar
Tuzo za All Africa Music Award, zinazofanyika kila mwaka, zimeorodhesha majina ya wasanii mbalimbali ambao kwa mwaka 2021 watatunishana misuli katikia vipengele 38 tofauti!
Kwa upande wa Tanzania, wasanii kadhaa wametajwa kuwania tuzo hizo:
Nandy; Anawania katika kipengele cha Mwanamuziki bora wa kike ukanda wa Afrika mashariki, kupitia wimbo wake wa Nimekuzoea, akichuana na wasanii wenzake kutoka Tanzania akiwemo; Rosa Ree kupitia wimbo wake wa That Gal, Spice Diana, Body pamoja na Zuchu kupitia wimbo wake wa Sukari na wasanii mbalimbali kutoka mataifa tofauti!
Katika kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume ukanda wa Afrika Mashariki, kuna Watanzania kama: Darassa kupitia wimbo wake wa Proud of you, Diamond Platnumz kupitia wimbo wake wa Waah, Harmonize kupitia wimbo wake wa Attitude pamoja na Rayvany kupitia wimbo wake wa Kelebe, pamoja na Harmonize huku wakichuana na wasanii kibao kutoka mataifa tofauti!
Katika kipengele cha Msanii ambae ni kipenzi/ chaguo la mashabiki , Mtanzania pekee ambae ni Ali Kiba anachuana na wasanii kutoka mataifa kama; Nigeria, Ivory Cost na DRC kupitia wimbo wake wa Jealous!
Huku katika kipengele cha Msanii bora wa mwaka, Diamond Platnumz , ni msanii pekee anayewania kipengele hicho huku akichuana na wasanii kama: Burnaboy, Davido na Wizkid.
Katika kipengele cha DJ bora, Mtanzania pekee ni Dj Sinyorita huku akichuana na Madj wakali kutoka ,Nigeria, South Africa na Ghana.
Director Kenny, anawania kipengele cha Video bora ya mwaka , kupitia video ya Waah ya Diamond, huku akichuana na waongozaji video (Video Director) kutoka: Nigeria, Kenya , Cape Varde na Egypt.
Katika kipengele cha Msanii bora upande wa rege na miondoko ya raga, Rosa Ree ni Mtanzania pekee ambae amechaguliwa kupitia wimbo wake wa That Gal. Pia Rosa Ree amechaguliwa katika kipengele cha Mwanamuziki bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Satan.
Rayvany na Diamond Platnumz wanawania pia katika kipengele cha wasanii bora upande wa uchezaji katika video zao.
Katika kipengele cha msanii aliyevunja rekodi ya mwaka, Zuchu kupitia wimbo wa Sukari anachuana na wasanii wengine kutoka mataifa tofauti.
Mtayarishaji bora wa mwaka (Music Producer), Laizer kutoka Tanzania kupitia wimbo wa Waah anachuana na watayarishaji wengine wa mataifa tofauti!.
Wimbo bora wa mwaka, msanii Diamond kupitia wimbo wake wa Waah pamoja na Rayvany kupitia wimbo wake wa Number One, wanatunishana misuri na wasanii wengine kama ; Wizkid, Patoranking , Davido na wengine wengi.
Huku kipengele cha nyimbo bora Afrika walioshirikishana, Diamond kupitia Waah aliyomshirikisha Kofi Olomide anachuana na Nandy kupitia wimbo wake wa Number One alomshirikisha Joeboy huku wakichuana na mastaa wengine wengi kutoka mataifa mbalimbali.