MICHAEL K. WILLIAMS: ALIFARIKI KWA KUZIDISHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
Na Bakari Mahundu, Dar
Muigizaji mkongwe katika filamu mbalimbali zikiwemo; The Wire na Boardwalk Empire, alifariki kutokana na kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya, ripoti za uchunguzi wa Kidaktari zimeeleza.
Michael ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 54, mwili wake ulikutwa nyumbani kwake, Brooklyn , Septemba 6. Ripoti za awali za Polisi zilieleza kuwa kulikuwepo na vifaa vya dawa za kulevya katika eneo ambalo mwili wa Michael ulipatikana.
Kipindi cha uhai wake, Williams; Amewahi kuteuliwa kushiriki katika Tuzo za Filamu za Emmy na aliwahi kuibuka mshindi katika Tuzo zilizotolewa na Netflix 2019 kupitia uhusika wake aliocheza katika Filamu.
Toa Maoni Yako Hapa