FACEBOOK IMESITISHA PROGRAMU YA WATOTO KATIKA MTANDAO WAKE WA INSTAGRAM
Na Bakari Mahundu
Kampuni ya kimataifa ya Facebook, imetangaza kusimamisha mradi wake unaohusu watoto kupitia mtandao wake wa Instagram, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wanaharakati wa haki za watoto na mamlaka mbalimbali.
Facebook ambayo ni kampuni mama ya Instagram, ilianzisha mradi huo kwa lengo la kuwawezesha watoto wenye umri chini ya miaka 13 kutumia mtandao huo wa Instagram, huku wakipata maudhui yanayolingana na umri wao.
Hili linakuja siku chache baada vyombo mbalimbali vya habari vya nchini Marekani, kulipoti tuhuma zinasoonesha programu hiyo ya watoto katika mtandao wa Instagram kuwa na madhara kwa ustawi wa watoto wakike.
Toa Maoni Yako Hapa