Sambaza

R-KELLY:  KIFUNGO CHA MAISHA CHANUKIA KWA UDHALILISHAJI WA KINGONO

Na Bakari Mahundu, Dar

Mwimbaji wa Marekani R Kelly  huenda akahukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia hadhi yake ya kuwa nyota wa muziki wa RnB kuendesha mpango wa kuwadhulumu kingono wanawake na watoto kwa zaidi ya miongo miwili.

Wahanga 11 wakiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, waliielezea Mahakama juu ya namna Staa huyo mkubwa Duniani, alivyowatumia na kuwadhalilisha kingono. Baada ya siku mbili ya majadiliano, jaji alimpata R Kelly na hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa anakabiliwa nayo.

Majaji walimpata Kelly, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, kuwa kiongozi wa mpango hatari uliyowavutia wanawake na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono. Mwimbaji huyo – maaarufu wa wimbo wa I Believe I Can Fly ulioshinda tuzo , pia aligundulika kuwasafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani na kuandaa filamu ya ngono ya watoto.

Hukumu dhidi yake itatolewa Mei 4 na huenda akafungwa maisha

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey