Sambaza

RAIS ACHUKIZWA NA ULAJI WA MBWA

Na Bakari Mahundu, Dar

Rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in anaangalia ikiwa sasa ni muda sahihi wa kupiga marufuku ulaji wa mbwa nchini humo.

Rais Moon ambaye amekuwa mfugaji wa mbwa kwa miaka mingi huku akiwa na mapenzi kwa viumbe hivyo, ameonesha nia ya kupiga marufuku ulaji wa mbwa ikiwa ni mkakati wa kulinda wanyama hao nchini humo.

Kulingana na takwimu za nchini Korea Kusini, zinaonesha kushuka kwa ulaji wa nyama ya mbwa na paka huku takribani mbwa milioni moja wanachinjwa kwa mwaka katika nchi hiyo. Hatua za awali zilizowahi kuchukuliwa ni pamoja na kupiga marufuku uchinjaji wa kikatili unaofanywa dhidi ya wanyama hao.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey