Sambaza

Tyga Azungumza Baada ya Tuhuma za Kumpiga Aliyekuwa Mpenzi Wake

Na Bakari Mahundu, Dar

Rapa, muimbaji na muandishi wa nyimbo za Hip Hop, Micheal Ray Stevenson maarufu kama Tyga, amevunja ukimya juu ya tuhuma zinazomkabili za kumpiga mpenzi wake, Camaryn Swanson.

Jumanne ya wiki iliyopita, Tyga alijisalimisha Kituo Cha Polisi cha Los Angeles nchini Marekani baada ya aliyekuwa mpenzi wake Camaryn kufungua mashtaka kuwa;  staa huyo amemshushia kichapo na kumsababishia majeraha.

Taarifa za kipolisi zimeonesha , Tyga alishikiliwa Oktoba 12, 2021 na kisha kuachiliwa saa chache baadaye kwa dhamana ya dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100 za Kitanzania.

Kufuatia tetesi za tuhuma hizo kuzagaa mitandaoni, Tyga amekuja juu na kuzikanusha tuhuma hizo dhidi yake.

Tyga kupitia mtandao wa Instagram aliandika: I want everyone to know that the allegations against me are false. I was not arrested ,I took myself into the police station and cooperated. I have not been charged with any crime.”  (Nataka kila mmoja ajue kuwa tuhuma dhidi yangu ni za uongo. Sikukamatwa, nilijisalimisha mwenyewe kituo cha polisi na kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika. Sijashtakiwa kwa uhalifu wowote)

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey